Kuhusu Waandishi

Dr. Gabriel L. Upunda - MD; M. Med; MPH

Dr G. L. Upunda alisomea Udaktari katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (1972), Alimaliza masomo ya uzamili katika Kutibu (Internal Medicine) mwaka 1978) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na mwaka 1993 alimaliza mafunzo ya uzamili (Masters in Pubic Health) huko Johns Hopkins School of Public Health, USA. Amekuwa Mganga wa Wilaya, Mganga wa Mkoa (mara mbili), nakwa zaidi ya miaka kumi na tano amekuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kama kiongozi wa Afya Ya Msingi, Mkurugenzi wa Tiba na hatimae alikuwa Mganga Mkuu Wa Serikali kwa takriban miaka kumi. Dr G L Upunda amefanya kazi pia Shirika La Afya Ulimwenguni (WHO - AFRO).

Dr. Bashir Admani - M.B.Ch.B; M. Med (Paediatrics), C. Neph. (Paed)

Dr Bashir Admani alimaliza mafunzo yake ya Udaktari (1998) na kufanya mafunzo ya uzamili katika fani ya watoto (2004) kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya. Alipata mafunzo maalumu ya ubingwa wa juu katika magonjwa ya figo kwa watoto katika Red Cross Memorial Childrens’ Hospital, Cape Town, Afrika ya Kusini. Sasa hivi anafanya kazi ya Udaktari Bingwa wa Figo kwa Watoto katika Hospitali ya Chuo Kikuu Cha Aga Khan. Nairobi, Kenya. Yeye ni Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Figo kwa Watoto, Hospitali ya Nairobi. Wakati tunapoandika Dr Bashir Admani ni Katibu wa African Paediatric Nephrology Association (AFPNA).Aidha anatoa huduma zake pia kama Mweka Hazina wa Kenya Renal Association.

Dr. Sanjay Pandya - MD DNB (Nefrología).

Dr. Sanjay Panya ni Daktari Bingwa Mwandamizi wa Figo ambaye anafanya kazi Rajkot ( Gujarat – India). “Kidney Education Foundation” imeanzishwa naye ikiwa na kazi maalumu ya kusambaza ujumbe kwa watu wengi ili kuzuia na kutibu magonjwa ya figo.Kitabu cha FIGO kwa wagonjwa katika lugha za kiingereza, Hindi, Gujarat na Kutchi kimeandikwa naye. Kwa kushirikiana na timu ya madaktari bingwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, vitabu vya kuelimisha wagonjwa wa figo vimetayarishwa katika lugha zaidi ya 20. Ili kuwasaidia watu na wagonjwa wa figo wengi zaidi sehemu mbalimbali duniani, Dr Pandya na timu yake wameanzisha mtandao www.KidneyEducation.com. Kupitia mtandao huu unaweza kuvipata vitabu zaidi ya 230 katika zaidi ya lugha 20. Aidha katika miezi 60 watu wameingia kwenye tuvuti hii zaidi ya mara milioni 20. Kwa hivi sasa kitabu hiki kwa wagonjwa kinapatikana katika kiingereza, kichina, kihispania, kijapani, kiitalia, kihindi, kiarabu, kireno, kibangla, kiurdu na lugha nyingine kumi za kihindi.