24: Tatizo la kukoja Kitandani kwa watoto

Kukojoa kitandani
Hali hii huwa ni kawaida kwa watoto.Hali hii haisababishwi na ugonjwa wa figo, uvivu wala utukutu wa watoto wanavyokua. Mara nyingi tatizo hili huacha lenyewe, bila dawa, kadri mtoto anavyokua.Hata hivyo husumbua watoto na familia zao kwani huleta usumbufu na hata aibu.

Ni watoto wangapi hukojoa kitandani na huacha katika umri upi?

Kukojoa kitandani ni kawaida hasa katika umri wa chini ya miaka sita.Katika umri wa miaka mitano asilimia kumi na tano hadi ishirini hukojoa kitandani. Hali hii hupungua kadri miaka ya watoto inavyoongezeka Watoto wa miaka kumi ni asilimia tano tu wanaokojoa na katika miaka kumi na mitano ni takriban asilimia mbili wakati watu wazima ni kama asilimia moja tu huwa wanakojoa kitandani.

Ni watoto wapi hukojoa kitandani?

  • Watoto ambao wazazi wao walikuwa na shida hiyo hiyo wakiwa wadogo.
  • Watoto ambao wana matatizo ya kimaumbile hivi kwamba hawajui wanapotaka kukojoa.
  • Watoto wenye usingizi mzito.
  • Ni hali inayowapata sana wavulana kuliko wasichana.
  • Hali hii huzidishwa na usumbufu wa akili au wa kiafya.
  • Kwa watoto wachache (2 -3%),shida za kimwili kama maambukizo, kisukari, figo kudhoofika, minyoo, kufunga choo, kibofu kidogo, kasoro za uti wa mgongo au kasoro katika kilango cha yurethra kwa wavulana huwa chanzo cha shida hii.
Kitanda kwenda haja ndogo machafuko wakati wa usiku ni tatizo la kawaida kwa watoto wadogo , lakini siyo ugonjwa

Ni uchunguzi upi hufanywe na hufanywe lini?

Uchunguzi hufanywe kwa watoto wachache ambao wanashukiwa kuwa na kasoro za kiafya au za kimaumbi le zinazosababisha kujikojolea.Uchunguzi wa kawaida huwa wa mkojo, sukari, eksirei za mgongo na picha za kibofu na figo kwa kutumia ultrasound na picha nyingine za kitaalamu ili kuona figo na kibofu.

Matibabu
Mtoto huwa hajikojolei kwa kutaka kwa hivyo usimkemee, kumuadhibu wala kumchapa. Badada yake mtie moyo ya kwamba hali hii itaisha au kutibiwa.Matibabu ya kwanza huwa ni mafunzo na kubadilisha mazoea ya kunywa maji na kukojoa.Ikiwa hatua hizi hazimsaidii basi jaribu kumwekea saa ya kengele ili imwamshe au apewe dawa zinazoweza kujaribiwa.

1. Mafunzo na motisha

  • Lazima mtoto apewe mafunzo kuhusu kukojoa kitandani.
  • Si kwa kutaka mtoto anakojoa kitandani kwa hiyo usikasirike wala kumlaumu mtoto, kwani itazidisha hali hii.
  • Tahadhari mtoto asichekwe na wengine.
  • Ni muhimu kumsaidia mtoto kwa kumuonyesha kuwa familia yake iko pamoja naye na hali hii si ya kudumu.
  • Tumia nepi ambazo hutupwa na ambazo hufanana na chupi.Usitumie diapers.
  • Hakikisha kuna mwangaza usiku ili mtoto aweze kwenda kujisaidia kwa urahisi.
Kuzuia vinywaji usiku , Awe na mazoea ya kukojoa wakati fulani ni muhimu.

  • Weka nguo za kulalia, shuka za kitanda na taulo, ili iwe rahisi kubadilisha kama mtoto akiamshwa/akiamka na kuona kuwa nguo zake zimelowa kwa mkojo.
  • Funika godoro kwa plastiki ili lisilowe na mkojo.
  • Weka taulo chini ya shuka ya kitanda.ili kama kuna mkojo umepitiliza ukaushwe na taulo hilo.
  • Hakikisha mtoto anaoga kila asubuhi ili asiwe na harufu ya mkojo.
  • Msifu na kumtunza mwanao asipokojoa usiku.Hata zawadi ndogo humpa motisha.
  • Kutokupata choo kushughulikiwe. Ikiwa ni lazima apewe dawa.

2. Zuia vinywaji

  • Zuia kiasi cha vinywaji saa mbili au tatu kabla ya kulala.Hakikisha mtoto anakunywa maji ya kutosha wakati wa mchana.
  • Zuia kahawa, chai, soda au chokoleti jioni.Hivi huzidisha haja ya kukojoa usiku.

3. Ushauri wa mazoea ya kukojoa

  • Himiza mtoto akojoe mara mbili kabla ya kulala.kwanza kama kawaida kabla ya wakati wa kulala, na tena kabla ya kushikwa na usingizi.
  • Awe na mazoea ya kujisaidia wakati fulani kila siku.
  • Mtoto aamshwe kila baada ya saa tatu hivi baada ya kulala kila siku. Ikibidi tumia saa yenye kengele.
  • Jaribu kutathimini wakati ambapo mtoto hukojoa usiku ili umwamshe wakati huo.

Dawa husaidia mtu kutojikojolea kwa wakati zinapotumiwa lakini huwa haziponyeshi hali hii.

4. Kengele ya kuashiria kulowa

  • Hii ndiyo njia bora zaidi ya kuzuia kukojoa kitandani na hutumiwa kwa watoto wenye umri wa zaidi ya miaka saba.
  • Tone la kwanza la mkojo liangukapo,kengele hulia na kumwamsha mtoto hivyo basi anaweza kwenda kujisaidia. Kifaa hiki huwekwa kwenye nguo za ndani.
  • Saa yenye kengele umsaidia motto kuamka kabla tu hajakojoa.

5. Mazoezi ya kibofu

  • Watoto wengi wanaokojoa kitandani huwa na vibofu vidogo. Kibofu kinaweza kufanyishwa mazoezi ili kipanuke.
  • Wakati wa mchana watoto wananyweshwa maji mengi na kujikaza wasiende kukojoa wapatapo haja ya kwenda kukojoa.
  • Mazoezi haya humsaidia mtoto kuzuia mkojo kwa muda mrefu zaidi.Hii hufanya misuli ya kibofu ipate nguvu na kukiwezesha kibofu kuweka mkojo mwingi zaidi.

6. Matibabu ya dawa
Dawa huwa zinatumiwa tu kama njia zingine zote zimeshindwa. Hutumiwa kwa watoto walio na zaidi ya miaka saba. Hufanya kazi lakini haziponyeshi hali hii.Mtoto hurudia kukojoa kitandani dawa zikisimamishwa. Saa yenye kengele ni bora zaidi kuliko dawa.

A. Dawa za kuzuia mkojo ya DDAVP. : Dawa hizi hupatikana kwenye maduka na hutumiwa tu wakati njia zingine zimeshindwa. Dawa hizi hupunguza mkojo wakati wa usiku Kwa hiyodawa hii ina manufaa tu kwa watoto ambao wana mkojo mwingi.Mtoto anapopewa dawa hii asipewe vinywaji wakati wa jioni. Dawa hii hutolewa kabla ya kulala. Iwapo mtoto amekunywa maji mengi asipewe dawa hii .Ingawaje dawa hii inafanya kazi vizuri na athari zake ni kidogo, Wazazi wengi hawawezi kuinunua kwa sababu bei yake ni ghali.

Mtoto anayekojoa kitandani anafaa amwone daktari akijikojolea mchana, ana homa, anawashwa akikojoa na kushindwa kwenda choo.

B. Imipramin: ni dawa inayolegeza kibofu na kukaza kilango hivyo basi kuongeza uwezo wa kubeba mkojo.Dawa hii hutumiwa kwa miezi mitatu hadi sita.Hutumiwa saa moja kabla ya kulala.Ni dawa bora lakini kwa sababu ya athari zake haitumiwi sana.

C. Oxybutynini : Hii ina manufaa kwa watoto wanaojikojolea mchana.Hupunguza kubana kwa kibofu na kukiwezesha kupanuka.Athari zake ni pamoja na kukauka kinywa, uso kuwa mwekundu na kufunga choo.

Watoto wanaokojoa kitandani wanafaa kumwona daktari lini?

Familia ya mtoto imwone Daktari kama:

  • Anajikojolea mchana.
  • Anaendelea kujikojolea baada ya umri wa miaka saba au minane.
  • Anashindwa kuzuia choo.
  • Ana homa, maumivu, kuwashwa na kukojoa mara nyingi, kiu kingi na kuvimba uso na miguu.
  • Mkojo kutiririka polepole au kushindwa kukojoa.
  • Anaanza kukojoa tena baada ya kuacha kukojoa kitandani kwa walao muda wa miezi sita.