5: Magonjwa Makuu ya Figo

Magonjwa ya Figo yamegawanyika katika Makundi Mawili

  • Magonjwa yanayohitaji Matibabu:
  • Magonjwa ya figo yanayohitaji matibabu ni kama vile hitilafu ya figo, maambukizi ya mfumo wa mkojo na uvimbe wa mwili (nephrotic Syndrome) yanatibika na dawa na mtaalamu wa nefrolojia. Wagonjwa wenye hitilafu ya figo ambayo imekwisha kuwa sugu, wanahitaji matibabu ya dayalisisi na kubadilishwa/kupandikizwa figo.

  • Magonjwa yanayohitaji Upasuaji:
  • Wanaurolojia hutibu magonjwa ya upasuaji kama vile ugonjwa wa mawe, shida za uume na saratani ya mfumo wa mkojo kwa upasuaji, endoskopia na lithotripsia.

  • Kuna tofauti gani kati ya wana nefrolojia na wana urolojia?
  • Wana nefrolojia ni wataalamu wa matibabu na wana urolojia ni wapasuaji maalum wa magonjwa ya figo.

Magonjwa makuu ya figo
Magonjwa ya Kutibu Magonjwa ya Upasuaji
Hitilafu kali ya figo
Ugonjwa sugu wa figo
Maambukizi ya mfumo wa mkojo
Hitilafu za uvimbe (nephritic syndrome)
Ugonjwa wa mawe
Shida za uume
Hitilafu za kuzaliwa nazo za wa mkojo mfumo wa mkojo
Saratan
Upotevu wa kazi ya figo huendelea polepole na bila kurudi nyuma kwa muda mrefu. Tatizo hili huitwa ugonjwa sugu wa figo.

Figo Kushindwa Kufanya Kazi

Upungufu wa uwezo wa figo kuchuja na kutoa uchafu na kudhibiti msawazisho wa elektrolaiti huitwa kwa ujumla wake figo kushindwa kufanya kazi (Kidney failure). Ongezeko la kiwango cha kreatinini ya serani na yurea ya damu katika upimaji wa damu hutoa hisia na hatimae hudhihirisha hitilafu ya figo. Hitilafu ya figo imegawika katika aina mbili, hitilafu kali/ghafla ya figo na hitilafu sugu ya figo (ugonjwa sugu wa figo).

Figo kushindwa Kufanya Kazi Ghafla / Hitilafu kali ya figo

Upungufu wa ghafla au upotevu wa kazi ya figo ghafla huitwa hitilafu kali ya figo au jeraha kali ya figo (Acute Renal Injury AKI).

Wingi wa mkojo hupungua kwa wagonjwa wengi wenye hitilafu kali ya figo. Sababu nyingine muhimu za figo kuwa na hitilafu kali ni kuhara,kutapika, malaria,(hasa aina ya falciparum), msukumo wa(au shinikizo la) damu, maambukizi kwenye damu (sepsis),kushuka ghafla kwa presha ya damu (hypotension) dawa fulani fulani (ACE inhibitor NSAIDs) na kadhalika. Kwa matibabu bora na wakati mwingine kwa kutumia dayalisisi kazi ya figo hurudi kuwa kawaida.

Ugonjwa Sugu Ya Figo/Hitilafu Sugu Ya Figo

Upotevu wa kazi ya figo wa polepole unaweza kuendelea kwa miezi kadha hadi miaka huitwa ugonjwa sugu wa figo (Chronic Kidney Disease – CKD). Katika CKD utendaji kazi wa figo hupungua polepole na bila kukoma. Baada ya kipindi kirefu,hufanyaji kazi wake unapungua hadi pale figo hukoma kufanya kazi kabisa. Hatua hii inayotishia maisha inaitwa hatua ya mwisho ya ugonjwa wa figo. (End Stage Kidney (renal) Diaease - ESKD/ESRD).

Dayalisisi ni mbinu ya kuingwa au bandia ya kutoa uchafu na maji mengi ya ziada kutoka kwenye damu ikiwa figo limeshindwa kufanya kazi kabisa /limefeli kufanya kazi kabisa.

Ugonjwa sugu wa figo huja kimya kimya na hautambuliki. Hatua za mwanzo za CKD, ni uchovu, ukosefu wa hamu ya chakula, homa, uvimbe, msukumo wa /shinikizo la damu kupanda na kadhalika. Vyanzo viwili muhimu vya CKD ni kisukari na msukumo wa juu wa damu.

Kuwepo kwa protini kwenye uchunguzi wa mkojo, kreatinini kuwa juu kwenye damu na figo ndogo/ zilizosinyaa kwenye kjpimo cha sonografia ni vidokezo muhimu sana vya utambuzi wa ugonjwa sugu wa figo.Kiwango cha kreatinini ya serami huonyesha ukali wa hitilafu ya figo, na kadri kiwango cha kreatinini kinavyoongezeka ndivyo maendeleo katika ugonjwa huwa mabaya zaidi.

Katika hatua za mwanzo za CKD, mgonjwa anahitaji dawa na uchaguzi bora wa lishe. Hakuna matibabu yanayoweza kuponyesha ugonjwa huu. Aidha nia ya matibabu iwe kupunguza mserereko na matatizo mengine (complications) ya ugonjwa huu na hivyo kumweka mgonjwa katika hali nzuri kwa muda mrefu na maradhi yake licha ya kwamba ugonjwa wake ni mkali.

Ikiwa ugonjwa umeendelea hadi kiwango cha mwisho,( End Stage Kidney Disease), kwamba zaidi ya asili mia tisini(90%) ya kazi ya figo imepotea, kreatinini ya serami huwa zaidi ya 8-10 mg/dl. Njia pekee ya matibabu katika hatua hii ni dayalisisi: dayalisisi ya damu (haemo) na dayalisisi ya peritonia (peritoneal) na ubadilishaji wa figo.(kidney transplantation).

Dayaisisi ni njia ya pekee ya kutoa uchafu na maji mengi yanayokusanyika kwenye mwili wakati figo inapokoma kufanya kazi. Dayalisisi si tiba ya ugonjwa sugu wa figo. Katika hatua ya mwisho ya ugonjwa sugu wa figo, (ESKD), mgonjwa huhitaji matibabu ya dayalisisi ya mara kwa mara kwa maisha yake yote (labda tu kama figo imepandikizwa na imefaulu).

Kuchelewesha matibabu na kutomchunguza mtoto mwenye UTI kunaweza kusababisha uharibifu kabisa wa figo linalokua./ changa.

Mbinu mbili za dayalisisi ni himo - dayalisisi na dayalisisi peritoni. Himo - dayalisisi (HD) ndiyo aina inayotumika sana. Katika HD kwa usaidizi wa mashine maalumu, uchafu, maji mengi na ya ziada na chumvi chumvi hutolewa.

Dayalisisi ya kuendelea ya peritonia (Continuous Ambulatory Peritoneal Dialysis - CAPD) ni namna nyingine ya dayalisisi ambayo inaweza kufanywa nyumbani au katika sehemu za kazi bila matumizi ya ile mashine maalumu.

Kubadilisha figo ndiyo njia pekee na bora ya matibabu ya ugonjwa sugu wa figo wa hatua hii ya mwisho .

Maambukizi ya mfumo wa mkojo

Kuchoma na kukojoa kwingi, uchungu katika sehemu ya chini ya tumbo na homa ni dalili za kawaida za maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Upimaji wa mkojo utaonyesha kuwepo kwa chembe chembe za usaha kwenye mkojo.

Wagonjwa wengi wa UTI hupona vyema na dawa za kuuwa wadudu (antibiotic). UTI kwa watoto inahitaji kushughulikiwa kwa uangalifu mkubwa na maalum sana. Kuchelewesha matibabu au matibabu yasiyotosheleza ya UTI kwa watoto yanaweza kusababisha uharibifu kabisa wa figo linalokuwa.

Kwa wagonjwa wenye UTI unayojirudia rudia, ni muhimu kuona kama kuna shida kati ya hizi zilizotajwa hapa chini kwa uchunguzi zaidi:

  • Kizuizi katika njia nzima ya mkondo wa mkojo,
  • Ugonjwa wa mawe,
  • Hitilafu katika mfumo mzima wa njia ya mkojo (abnormality) na
  • Kifua kikuu cha mkojo

Chanzo kikuu cha UTI kujirudia rudia hasa kwa watoto ni mkojo kurudi nyuma (Vesicoureteral reflux - VUR). VUR ni hitilafu ya kuzaliwa nayo kwenye mfumo wa mkojo ambapo mkojo hurudi nyuma kutoka kwenye kibofu hadi kwenye ureta moja au zote na hata hadi kwenye figo.

Mawe ya figo yanaweza kuwepo bila dalili hata kwa miaka.

Uvimbe Wa Mwili ( Nephrotic Syndrome)

Uvimbe wa mwili ni ugonjwa wa figo unaoonekana mara nyingi kwa watoto ikilinganishwa na watu wazima.

Uvimbe wa kila mara (oedema) ndio dalili kubwa ya ugonjwa huu. Kuwepo kwa protini kwenye mkojo (zaidi ya grammu 3.5 kwa siku) kiwango cha chini cha albumin kwenye damu (haipoalbuminemia), kiwango cha juu cha cholesterol, msukumo wa kawaida wa damu na figo kufanya kazi kama kawaida ni baadhi ya dalili /sifa za ugonjwa huu.

Ugonjwa huu huonyesha matokeo mazuri kwa matibabu.Wagonjwa hubakia bila dalili baada ya kusitisha matibabu lakini mara nyingi, ugonjwa hujitokeza tena.

Tabia hii ya mzunguko ya ugonjwa kujirudia rudia na kuitikia matibabu kipindi cha matibabu, ndizo sifa/dalili za ugonjwa huu wa uvimbe wa mwili.

Jinsi ugonjwa unavyojirudia rudia kwa muda mrefu (miaka), ugonjwa huu ni suala la mahangaiko kwa mtoto pamoja na familia. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa matokeo ni ya kudumu na mazuri zaidi kwa watoto wenye uvimbe wa figo. Hatimae wanaishi maisha ya afya na ya kawaida wakiwa na figo zinazofanya kazi kama kawaida.

BPH ndicho chanzo cha kawaida cha shida za mkojo kwa wazee wa kiume.

Mawe Katika Figo

Mawe katika figo ni shida muhimu na ya kawaida ya figo. Figo, ureta, na kibofu ni sehemu ambazo mawe yanaweza kuwepo. Dalili za kawaida ni uchungu wa kupindukia,usiostahimilika, homa,kutapika, damu kwenye mkojo n,k. Hata hivyo, wapo watu wengine walio na mawe ya figo (hata kwa muda mrefu) hawana dalili zozote kabisa.

Kwa utambuzi wa mawe, eksirei ya tumbo na picha ya sonografia ni uchunguzi muhimu sana.

Mawe mengi madogo madogo hutoka tu pamoja na mkojo kwa kunywa vinywaji vingi/maji mengi.. Iwapo mawe yanasababisha maumivu mengi, maambukizi ya kurudia rudia, kuziba kwa mkondo wa mkojo au uharibifu wa figo, ni muhimu yaondolewe.. Mbinu ya kuyaondoa mawe hutegemea ukubwa, eneo na aina yake. Mbinu za kawaida ni lithotripsia, endoskopia (PCNL, sistoskopia na uretaskopia) na upasuaji wa wazi. Kwa vile hatari ya kurudia kwa mawe ni juu hadi 50-80%, unywaji wa maji mengi ,kudhibiti lishe na uchunguzi wa kila mara ni muhimu.

Tatizo la tezi dume la kibofu kupanuka (BPH)

Tezi dume hupatikana kwa wanaume. Huwa sehemu ya chini ya kibofu na huzunguka sehemu ya mwanzo ya uretha. Tezi dume huanza kupanuka baada ya umri wa miaka ya 50. Tezi dume iliyopanuka hufinya urethra na kusababisha shida kwa kukojoa kwa wazee wa kiume.

Dalili kuu za BPH ni kukojoa mara nyingi (hasa usiku) na mkojo kutoka kidogo kidogo baada ya kukojoa. Uchunguzi ni pamoja na kuweka kidole kwenye sehemu ya haja kubwa (rektamu), wa kidijitali na ultra sound ni njia mbili mzuri na kubwa za utambuzi wa BPH.

Idadi kubwa ya wagonjwa wenye dalili za chini au chache za BPH wanaweza kutibiwa vyema kwa kipindi kirefu kwa kutumia dawa. Wagonjwa wengine wenye dalili kali za kuwepo kwa tezi dume kubwa watahitaji kutolewa kwa tezi dume hilo (TURP).