21: Dawa na matatizo ya figo

Dawa za kutuliza maumivu

Kuna matatizo mengi ya figo yanayotokana na dawa.

Kwa nini figo hudhurika na dawa kuliko kiungo kingine chochote cha mwili?

Sababu muhimu za dawa kudhuru figo ni:

1. Figo ni kiungo kitoacho dawa mwilini: figo ndiyo huhusika katika kazi ya kuondoa dawa mwilini.Wakati dawa inapotolewa kuna uwezekano wa dawa au vitu vilivyoitengeneza kudhuru figo.

2. Damu nyingi kupitia kwenye figo: kwa kila dakika, asilimia ishirini ya damu ya mwili(mililita kama elfu moja mia mbili)huingia kwenye figo zote mbili ili kusafishwa. Ukilinganisha viungo vyote vya mwili, figo ndiyo hupokea damu nyingi kuliko vyote.Kwa sababu hiidawa na vitu vingine vingi vyenye madhara hupitia kwenye figo.Hii inaweza kudhuru figo.

Dawa zinazodhuru figo
1. Dawa za kutuliza maumivu

Maumivu ya mwili, kichwa, viungo na homa hutulizwa kwa dawa zinazopatikana hata madukani bila ushauri wa daktari (OTC). Dawa hizi hudhuru figo.

Kuna dawa nyingi za kupunguza maumivu na homa.Hizi ni kama aspirin,diclofenac,ibuprofen,indomethacin,ketoprofen,nimesulide,naproxen n.k.

Dawa za maumivu na homa hudhuru figo? (NSAIDs)

Dawa hizi huwa salama zikitumiwa kama daktari alivyoagiza.Kumbuka hizi ndizo nambari ya pili baada ya zile za antibayotiki,(za kutibu maambukizi)miongoni mwa dawa zinazodhuru figo.

Dawa za kutuliza maumivu ni chanzo kikuu cha madhara kwa figo.

Dawa (NSAIDs) za maumivu na homa hudhuru figo lini?

Hatari ya figo kudhurika ni kubwa kama:

  • Dawa za maumivu zikitumiwa kwa muda mrefu na kwa dozi kubwa bila ushauri wa daktari.
  • Matumizi ya muda mrefu ya dawa moja yenye mchanganyiko wa dawa kadhaa kama vile APC ambayo huwa na aspirini,fenasetini,na kafeini.
  • Matumizi ya dawa za maumivu kwa mtu mzee,figo dhoofu,kisukari au maji kidogo mwilini.

Ni dawa ya maumivu ipi inayofaa kwa wagonjwa wa figo?

Paracetamol au acetaminophen ndiyo dawa salama kuliko zingine.

Wagonjwa wa moyo hushauriwa kutumia aspirini maisha yao yote. Je, hii inaweza kudhuru figo?

Kwa kuwa kiasi kidogo sana cha aspirin kinashauriwa kumezwa na wagonjwa wa moyo, basi aspirin hiyo ni salama.

Je, ugonjwa wa figo unaosababishwa na dawa unaweza kutibiwa?

Ndio na La.

Ndio, kama madhara yamesababishwa na matumizi ya dawa kwa muda mfupi tu.Dawa zikisimamishwa na matibabu yanayofaa yakizingatiwa.
La, kama madhara yamesababishwa na matumizi ya dawa kwa muda mrefu.kama kwa mfano kwa watu wazee wenye maumivu ya viungo ambao huhitaji dawa kwa muda mrefu.Watu kama hawa wanafaa kuzitumia dawa hizi kwa kuzingatia ushauri wa daktari tu. Kiasi kidogo cha aspirin kinachoshauriwa kutumiwa na wagonjwa wa moyo ni muhimu, kinasaidia na ni salama.

Kujitibu na dawa za kawaida za kupunguza maumivu kunaweza kuwa hatari.

Jinsi ya kutambua madhara ya polepole yanayosababishwa na dawa za maumivu?

Protini kupatikana kwenye mkojo ndiyo dalili ya kwanza na ya pekee.Madhara yakizidi uchafu wa kreatinini huongezeka kwenye damu.

Njia za kuzuia figo kudhuriwa na dawa?

  • Usitumie dawa za maumivu kwani una uwezekano wa kuwa hatarini.
  • Usinunue dawa dukani wala kuzoea dawa hizi za maumivu.
  • Iwapo unahitaji dawa za maumivu kwa muda mrefu, sharti ufuate ushauri wa daktari.
  • Uwe na kikomo cha muda na dozi za dawa za maumivu.
  • Usitumie dawa zenye mchanganyiko wa dawa za kutuliza maumivu kwa muda mrefu.
  • Kunywa vinywaji kwa wingi ili kuhakikisha damu ya kutosha inaenda

kwenye figo na kuzuia figo kudhurika.

Hatari ya uharibifu wa figo unaoletwa na dawa ni mkubwa zaidi kwa wagonjwa wenye kisukari, figo lililofeli/lililoshindwakufanya kazi,kukosa maji mwilini na umri mkubwa (uzee).

Dawa za maambukizo aminoglycosides

2. Dawa za maambukizo (antibayotiki)aminoglycosides

Hizi ni dawa za kawaida na chanzo kingine cha figo kuharibika.Figo hudhurika baada ya kutumia dawa hizi kwa siku saba hadi kumi.Mara nyingi ugonjwa huu haujulikani kwani kiasi (volume) cha mkojo hakibadiliki.Hatari ya dawa hizi huzidi kwa walio na umri mkubwa,kukosa maji mwilini, wenye ugonjwa wa figo,kukosa potasiumu na magnesiamu,kutumia dawa hizi kwa muda mrefu,kutumia dawa hizi pamoja na zingine zinazoweza kudhuru figo,ugonjwa wa ini, wa moyo na maambukizi kwenye damu.

Jinsi ya kuzuia antibayotiki aminogycosides kudhuru figo?

  • Tahadhari ya matumizi ya dawa hizi kwa walio hatarini au kutibu hali inayowafanya wawe hatarini.
  • Kama ni lazima basi dozi itolewe mara moja kwa siku badala ya mara nyingi.
  • Tumia dozi sahihi na kwa muda unaofaa.
  • Rekebisha dozi kwa mtu ambaye tayari ana figo lenye kasoro.
  • Chunguzakiwango cha kreatinini kila siku ya pili ili kutambua tatizo mapema.
Kwa wagonjwa wenye hatari wape “aminoglycosides” kwa uangalifu sana huku ukipima kreatinini (serum creatinine) ili kuzuia uharibifu wa figo.

3. Sindano za eksirei

Rangi itumikayo katika picha za eksirei husababisha figo kushindwa kufanya kazi,kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini.Hali hii hupona.Hatari ya figo kuharibiwa na hii rangi huwa kubwa kwa wagonjwa wa kisukari,wagonjwa waliokosa maji ya kutosha mwilini,tatizo la moyo,figo iliyodhoofu,uzee na matumizi ya dawa yanayoweza kudhuru figo.Njia ya kuzuia figo kuharibiwa na rangi ya eksirei ni kutumia rangi kiasi, kuhakikisha mgonjwa ana maji ya kutosha mwilini kwa kumuongeza maji kwa njia ya mshipa,awe na magadi (sodium bicarbonate) na acetylcysteine.

4. Dawa zingine

Dawa zingine zinazoweza kudhuru figo ni antibayotiki fulani fulani, dawa za saratani, kifua kikuuna kadhalika.

5. Dawa nyingine

  • Imani kuwa dawa zote za asili kama vile dawa za miti na dawa za vyakula (food supplements) ni salama ni imani potovu.
  • Dawa nyingine kati ya hizi za asili huwa na madini mazito (heavy metals) na vitu vinavyoweza kudhuru figo.
  • Matumizi ya dawa hizi yanaweza kuwa hatari kwa wagonjwa wa figo.
  • Dawa nyingine zenye potasiumu nyingi zinaweza kuwa hatari hata kuleta kifo, kwa wagonjwa wenye figo zilizofeli.
Ni imani potovu kuwa dawa za kienyeji zote ni salama.